The House of Favourite Newspapers

Molinga Awatolea Kauli la Kibabe Simba SC

0

MSHAMBULIAJI tishio wa Yanga, Mkongomani, David Molinga ‘Falcao’, amewatolea kauli la kibabe wapinzani wao wakuu Simba kwa kuwaambia kuwa kwake hawamtishi hata kidogo na kuongeza kuwa wakikutana Januari 4, mwakani, wana uhakika wa kuchukua pointi tatu kutoka kwao.

 

Molinga ameweka wazi kwamba kwake hatishwi na Simba ambao ndiyo vinara wa ligi wakiwa na pointi 25 huku akiwafananisha na timu nyingine za ligi kuu.

 

Straika huyo aliyefunga mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, atacheza na Simba katika mechi ya watani ambayo itapigwa Januari 4, mwakani katika Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Straika huyo ameliambia Championi Jumatano kuwa kwake hawezi kuogopeshwa na Simba kwa sababu anawaona kama timu nyingine za ligi kuu ambazo wanakutana nao huku kwenye mechi hiyo akijipanga kuisaidia timu yake kupata pointi tatu.

 

“Hatuwezi kuwaogopa Simba, kwangu ni kama timu nyingine tu za ligi kama Mbeya City (ambao walicheza nao jana Jumanne) au timu nyingine za ligi kwa sababu zote tukishinda tunapata pointi tatu.

 

“Kitu kikubwa ambacho nitafanya tutakapokutana nao ni kuhakikisha timu yangu inapata matokeo mazuri kwa kushinda mechi yake, hicho ndiyo kitu cha muhimu na kimsingi kabisa niseme kwamba siwaogopi wao,” alimaliza straika huyo.

STORI NA Said Ally, Dar es Salaam

Leave A Reply