The House of Favourite Newspapers

Bosi Mkuu wa Kampuni ya X (zamani Twitter) India Samiran Gupta Ajiuzulu

0

Bosi Mkuu wa Kampuni ya X (zamani Twitter) nchini India Samiran Gupta amejiuzulu.

Hatua hiyo imekuja wakati Kampuni hiyo ikipambana Mahakamani na Serikali ya India kuhusu amri ya kuondoa maudhui.

Gupta ambaye amejiuzulu mwezi mmoja tu kabla ya uchaguzi alijiunga na Twitter nchini humo Februari mwaka jana, miezi michache kabla ya kampuni hiyo kununuliwa na Bilionea Elon Musk.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters,  vyanzo viwili vya kuaminika vimethibisha suala hilo, japo Gupta amekataa kutoa maoni yeyote juu ya hilo.

Ni mtaalamu mkongwe wa masuala ya Mawasiliano, kabla ya kujiunga na Twitter alifanya kazi kwenye taasisi ya Kimataifa ya Mawasiliano (ICANN) kwa miaka 7.

X ina kesi mahakamani kwa kile ambacho serikali ya India imekiita kuwa ni “kutotii amri ya kuondoa maudhui”.

VIDEO: MADUDU KIGOMA, WAZIRI MKUU MAJALIWA AMWAGIZA MCHENGERWA AENDE KIGOMA KUCHUKUA HATUA…

Leave A Reply