The House of Favourite Newspapers

Bosi Yanga: Nini Maxi Nzengeli? Hamjamuona Pacome Zouzoua Nyinyi

0
Maxi Nzengeli.

BAADA ya mashabiki wa Yanga kupagawa na uwezo ambao ameuonyesha kiungo wao Maxi Mpia katika mechi dhidi ya Kaizer Chief sasa uongozi wa Yanga umesema kuwa kuna balaa jipya mashabiki hawajaliona kutoka kwa kiungo wao Pacome Zouzoua.

Pacome katika mechi dhidi ya Kaizer Chiefs hakufanikiwa kucheza kutokana na kutokuwa fiti huku Maxi na wachezaji wengine wote wapya wakifanikiwa kucheza na kuonyesha ufundi wao mbele ya Wananchi.

Pacome Zouzoua.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema: “Wamemuona Maxi Nzengeli akifanya yake lakini niwaambie tu jambo moja kuwa hawajabahatika kumuona yule Pacome Zouzoua.

“Yule ni moja kati ya wachezaji ambao wamekamilika sana na naamini siku wakimuona aanacheza watapagawa kwani ni moja kati ya wachezaji mwenye uwezo mkubwa sana wa kupambana ndani ya uwanja.

“Msimu ujao niwaambie tu Yanga itakuwa kwa staili nyingine mpya ambayo watu watakuja kuifahamu wakiwa wamechelewa sana, hivyo tunaamini chini ya kocha Gamondi kuwa tutafanya vyema na tutayapigania mataji yetu,” alisema kiongozi huyo.

ABBAS TARIMBA AFUNGUKA SAKATA la MAYELE KUUZWA – “NIMEFURAHI, FEI TOTO SIJAKUBALIANA NAYE”..

Leave A Reply