The House of Favourite Newspapers

BoT Yaikana Pesa ya Mtandaoni, Yatoa Onyo

0

BENKI Kuu nchini imeonya kuacha mara moja kujihusisha na shughuli za fedha za kimtandao (Cryptocurrency) kunakofanywa na baadhi ya watu wanaojihusisha na bishara hiyo haramu.

 

Imeeleza kuwa watu hao wanaoleta usumbufu ndani na nje ya nchi, wamekuwa wakidai kuwa shughuli zao zinaungwa mkono na Benki Kuu ya Tanzania jambo ambalo halina ukweli wowote.

 

Novemba 12, benki hiyo ilitoa taarifa kwa umma ikiwataka wananchi kujiepusha na uuzaji, uhamishaji na matumizi ya fedha za kimtandao kwani kufanya hiyo ni kinyume cha Kanuni za Udhibiti wa Fedha za Kigeni.

Leave A Reply