The House of Favourite Newspapers

BOT YAPONGEZA HUDUMA MPYA YA NMB

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker,  akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za benki hiyo.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imepongeza mfumo wa mabadiliko ya kidijitali unaoendelea kuboreshwa katika Benki ya NMB huku ikiahidi kusapoti mapinduzi hayo ya kimfumo ili kupunguza idadi ya Watanzania wasiotumia huduma za kibenki.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse, wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma tatu za Benki ya NMB, ikiwemo ya ufunguaji wa akaunti ya benki kwa kutumia simu ya mkononi.

Mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT), Bernard Kibesse akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni  jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Gavana Bernard Kibesse, ambako pamoja na ufuanguaji wa akaunti, pia amezindua App mpya iitwayo NMB Klik na NMB Scan Pay, ikiwa ni muendelezo wa maboresho ya kidijitali.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Gavana Kibesse amesema mchakato wa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa Kati unahitaji ubunifu wa kihuduma hususani kwa taasisi na kifedha na kwamba katika hilo NMB imejipambananua.

Alibainisha kwamba, mfumo wa kidijitali unaozidi kuboreshwa na NMB ni kati ya mabadiliko ya aina yake kuwahi kufanywa na taasisi
za kifedha nchini na kwamba BoT haitosita kuisapoti NMB katika kufikia malengo yake kidijitali iliyojiwekea.

 

“Sisi  kama benki kuu (BOT) tunaahidi ushirikiano kwa NMB na  siyo tu kufikia malengo yao, bali pia katika kuhakikisha inapunguza idadi ya Watanzania wasiotumia huduma za kibenki. Mandeleo kuelekea Uchumi wa Kati, yanahitaji ushiriki wa kila Mtanzania,” alisema Dkt. Bernard Kibesse.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema uzinduzi wa huduma hizo ni nafasi nyingine ya NMB
kuboresha huduma zake matawini na nje ya matawi na kwamba wamejipanga kuwafikia Watanzania popote walipo.

..Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya huduma hizo  mpya za benki.

Aliongeza kwamba wanajivunia mabadiliko ya kimfumo yanayofanya upatikanaji wa huduma uwe mikononi mwa Watanzania popote walipo na kwamba anaamini NMB Klik App, NMB Scan Pay na ufunguaji akaunti kwa simu za mkononi, utachagiza maendeleo yao.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Alisisitiza kuwa, katika kuhakikisha wanabaki kuwa kinara wa huduma za kibenki nchini, watahakikisha wanapokea na kuufanyia kazi
ushauri wowote watakaopata kutoka kwa wateja, ambao watabaki kuwa kipaumbele chao katika kuanzisha huduma mpya.

Ili kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi, mteja atapaswa kutembelea menu ya NMB Mobile, ambako atafuata maelekezo na kwa
watumiaji wa simu za Android na Iphone watapakua App ya NMB Klik kupitia Google Play Store na App Store.

App ya NMB KLiK inapatikana katika Playstore
https://goo.gl/Fr9fZf na kupitia AppStore https://goo.gl/wQXZV6

 

Comments are closed.