The House of Favourite Newspapers

BREAKING: NONDO ASHINDA KESI YA ‘KUJITEKA’, AACHIWA HURU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo, leo Jumatatu, Novemba 5, 2018, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa ya mshitakiwa.

 

Katika kesi hiyo ambayo Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kutekwa na kutoa taarifa za uongo, mahakama hiyo imemkuta hana hatia baada ya baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kueleza mshitakiwa alifikaje Mafinga.

 

Aidha, mahakama imesema hakuna ushahidi kutoka upande wa Jamhuri kuwa mshitakiwa alikuwa wapi wakati wa tukio na kuifanya mahakama ikose ushahidi, hivyo upande wa mashitaka kuonekana wametoa ushadidi wa hisia na hivyo kuamua kumuachia huru.

SERIKALI YAMPINGA MAKONDA KUHUSU USHOGA “Tuna Mikataba”

Comments are closed.