The House of Favourite Newspapers

Breaking: Basi la Emigrace Lapata Ajali – Video

0

Basi la Kampuni ya Emigrace lenye namba za usajili T 703 DLG linalofanya safari zake kati ya Babati na Dar es Salaam, limepata ajali leo asubuhi katika mlima wa Kolo, Kata ya Kolo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

 

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu saba wamepoteza maisha papo hapo ambapo kati yao ni wanaume watu wazima wawili na mtoto mmoja wa kiume, wanawake wawili na watoto wawili wa kike na majeruhi zaidi ya 30.

 

Inaelezwa kuwa, miili ya watu hao imepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Kondoa huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa katika hospitali hiyo na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Mrara, Halmashauri ya Mji wa Babati.

 

Global TV imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Dodoma lakini simu yake imeita muda mrefu bila kupokelewa. Jitihada zaidi zinaendelea. Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi amina.

 

 

 

Leave A Reply