Simba Watoa Tamko kwa Viongozi Wanaotoa Ahadi

MSHAURI wa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crecentius Magori amewataka Viongozi  wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa wasitoe hela na waache timu zicheze mpira kwakuwa anaamini timu yenye uwezo itapata matokeo.

 

Kauli hiyo imetolewa baada ya mchezo wa jana kushuhudiwa beki wa Simba, Kennedy Juma kufanyiwa rafu na mchezaji wa Dodoma Jiji na kushindwa kumaliza mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa wekundu wa msimbazi kushinda bao 1-0.

 

”Tunasikia watu wanaagiza mahela, naskia Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, ndio yanasabisha watu wanakamia mechi hata kama hawana uwezo lakini wanaharibu mpira,” amesema Crecentius Magori.

 

Katika mchezo wa jana wachezaji watatu wa Simba, Ousmane Sakho, Thaddeo Lwanga na Kennedy Juma hawakumaliza mchezo kutokana na majeraha.

 

Simba inakamata usukani wa Ligi Kuu ikiwa na alama 4 baada ya kucheza michezo miwili iliyocheza ikiwa imepata ushindi mmoja na sare moja.


Toa comment