The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Dkt. Malisa Awalipua CHADEMA, CCM Uchaguzi Kinondoni – Video

Dkt. Godfrey Malisa akizungumza na wanahabari.

 

MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya TLP, Dkt. Godfrey Malisa amewataka wananchi wa wa Jimbo hilo kuwakataa wagombea wa CCM, Maulid Mtulia na Salum Mwalimu wa CHADEMA kwa madai kuwa hawaaminiki kuwapa uongozi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za TLP Jimbo la Kinondoni, mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani nchini amesema, wagombea wote wawili hawaaminiki kutokana na kuyumbishwa katika misimamo yao. Amesema mgombea wa CCM, Maulid Mtulia, Dkt Malisa amedai haaminiki tena kwani ameonekana kutokuwa na msimamo madhubuti na amewasaliti wananchi wa Kinondoni kwa kuachia nafasi aliyo nayo na kurejea tena.

 

Dkt Malisa amedai hata CHADEMA haina nia madhubuti ya kuongoza jimbo hilo kwani imeonesha kuwasaliti Wana-Kinondoni kwa kuweka kando maamuzi yao ya mwaka 2015 na kuwaunga mkono CUF ambao nao wameshindwa kuwatumikia badala yake amewakimbia.

 

Dkt. Malisa ambaye ni mwanasiasa wa muda mrefu amevitaka vyombo vya habari kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote ili wananchi wapate fursa ya kuwafahamu wagombea wote na kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura.

VIDEO: MSIKIE MALISA AKIFUNGUKA

Comments are closed.