The House of Favourite Newspapers

BREAKING: JPM AWATUMBUA TIZEBA, MWIJAGE, AMTEUA WAITARA

Rais Dkt. John Magufuli leo Jumamosi, Novemba 10, 2018 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza lake la Mawaziri ambapo ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, nafasi yake inachukuliwa na Japhet Hasunga.

Rais ametengua Uteuzi wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Charles Mwijage nafasi yake inachukuliwa na Joseph Kakunda.

Pia, Magufuli amemteua Mbunge wa Ukonga,Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tamisemi.

 

FUATILIA UTEUZI HUO HAPA – VIDEO

Comments are closed.