The House of Favourite Newspapers

Breaking: Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Ajiuzulu – Video

RAIS  John  Magufuli  amesema Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amemwandikia barua ya kujiuzulu nafasi yake hiyo.

 

Hayo ameyasema katika Gereza la Ukonga wakati akifungua rasmi nyumba za  maofisa na wafanyakazi wa gereza hilo jijini Dar es Salaam ambazo zimejengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 

“Katika Wizara zinazonitesa, mojawapo ni hii ya Mambo ya Ndani. Tume nyingi zimeundwa kuchunguza miradi ya hovyo katika wizara hiyo. Ninajua hayupo hapa (Meja Jenerali Jacob Kingu) ameshaleta barua ya kujiuzulu, nimeshamkubalia na ninampongeza sana.

 

“Najua Waziri Lugola unafanya kazi kubwa, umejenga nyumba nyingi za polisi hata Chato umejenga, lakini hili la kwenda Ulaya kusaini mkataba wa mradi ambao hata haujapitishwa na bunge, kwa hili hapana! Ninashangaa kwa nini upo hapa. 

 

“Kamishina Jenerali Thobias Andengenye nampenda sana, lakini kwa hili hapana, nilitegemea hapa hayupo, hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya ajabu namna hii. Sitaki kuwa mnafiki, nitaendelea kuwapenda lakini kwenye position hii no,” alisema Magufuli ambapo alielezea kasoro kadhaa za utendaji katika jeshi la Magereza na Wizara ya Mambo ya Ndani.

 

Comments are closed.