The House of Favourite Newspapers

Breaking: Kaze Atimuliwa Yanga, Benchi la Ufundi Lavunjwa

0

BAADA ya kuanza vibaya kwa timu yao katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, uongozi wa klabu ya Yanga  leo Machi 7, 2021 umeamua kulivunja benchi lake la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Cedric Kaze.

 

Yanga imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania ambayo ilikuwa ni mechi ya sita kwenye mzunguko wa pili wakiambulia pointi saba pekee wakidondosha alama 11 baada ya kushinda mechi moja, sare nne na kipigo moja.

 

Kaze tangu akabidhiwe timu hiyo ameongoza mechi 18 akishinda 10, sare 7 na amepoteza 1.

Uongozi wa klabu hiyo umewataka wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo katika kipindi ambacho wanafanya utaratibu wa kupata benchi jipya.

Tangu kuanza kwa mzunguko wa pili yanga imecheza ugenini dhidi ya Prisons na kutoka sare ya bao 1-1, Mbeya City 1-1, Kagera Sugar 3-3, ikashinda dhidi ya Mtibwa 1- 0 na kufungwa na Coastal Union mabao 2-1.

Leave A Reply