The House of Favourite Newspapers

Breaking: Kimenuka! Kubenea, Komu Wavuliwa Uongozi – Video

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini), wamevuliwa nyadhifa zao zote ndani ya chama hicho, kupewa onyo kali na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja kuhusu nyendo zao katika chama hicho.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kuwahoji katika kikao kirefu, inahusu ujumbe wa sauti wenye mazungumzo yao dhidi ya chama hicho ulionaswa na kusambazwa katika mitandao hivi karibuni.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chadema – Bara, John Mnyika, amesema baada ya kuitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza, Kubenea na Komu walikiri kuwa sauti zilizosikika ni za kwao na baada ya mahojiano ya muda mrefu kamati hiyo iliamua kuwapa onyo kali, kuwavua nyadhifa zao zote ndani ya chama na kubakiwa na ubunge pekee.

 

“Clip ya sauti iliyosambaa mitandaoni ikiwahusisha wabunge wa Chadema, Anthony Komu na Saed Kubenea ilianzia kwenye grupu la WhatsApp la Chadema Kaskazini, hii inaashiria utovu mkubwa wa nidhamu kwa wabunge hao, waliitwa kuhojiwa mbele ya Kamati Kuu ya chama, walikiri kuwa sauti zilizosambaa ni za kwao, hivyo walikutwa na hatia ya kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama, kamati ilifanya maamuzi ya kuwaadhibu,” alisema Mnyika.

 

Aliongeza kwamba Kamati Kuu pamoja na kuwapa onyo kali wametakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kwa chama na wanaotajwa kwenye clip hiyo.

 

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.