The House of Favourite Newspapers

Breaking: Wawili Wajeruhiwa Lori la Soda Likigongana na Daladala

WATU wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kutokea ajali iliyohusisha lori lililokuwa limebeba soda, mali ya Kampuni ya Coca-Cola kugongana na basi la abiria (daladala) katika maeneo ya Mabibo Gereji jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Jumatano, Oktoba 2, 2019.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya breki kwenye lori hilo la soda na kumshinda dereva wake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa, amefika katika eneo la tukio na kujionea ajali hiyo ambapo amesema Jeshi la Polisi linachunguza zaidi na litatoa taarifa baadaye.

Endelea kufuatilia taarifa zetu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.