The House of Favourite Newspapers

Breaking: Mahakama Yaamua Musiba Kumlipa Membe Bilioni 6

0
Aliyekuwa Waziri mambo ya nje, Bernard Membe.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania,  imemuamuru Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kumlipa aliyekuwa Waziri mambo ya nje, Bernard Membe kiasi cha Sh. bilioni 6 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

 

Hukumu hiyo ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018, imetolewa leo tarehe 28 Oktoba, 2021 na Jaji Joacquine De Mello.

 

Amesema pamoja na Musiba kutakiwa kumlipa Membe Sh bilioni sita, pia ametakiwa kulipia gharama za kesi hiyo.
Amesema hukumu hiyo pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.

Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba.

Amesema katika kiasi hicho cha Sh bilioni sita, Sh bilioni tano ni fidia ya hasara halisi na Sh. bilioni moja hasara ya jumla.

 

Katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo aliwadai Sh. bilioni 10.3 kwa kumchafua.

 

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli (wakati huo) asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

 

Pia alidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi aliyokuwa akifanya ya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

 

Leave A Reply