The House of Favourite Newspapers

Breaking: Mahakama Kuu Arusha Yamuachia huru Sabaya na Wenzake Wawili

0

 

MAHAKAMA Kuu ya Kanda ya Arusha leo Mei 6, 2022 imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwa sababu mbalimbali kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.

 

Jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Hata hivyo,  Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Leave A Reply