The House of Favourite Newspapers

Mourinho Aweka Rekodi, Atinga Fainali Tatu Kubwa Ulaya

0
Kocha wa AS Roma Jose Mourinho

KOCHA wa sasa wa Klabu ya AS Roma ya nchini Italia Jose Mourinho maarufu kama ‘The Special One’ raia wa Ureno ambaye aliwahi kuvifundisha vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo  FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs ameweka rekodi mpya barani humo.

 

Mourinho ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kufika katika fainali za Ligi ya Mabingwa (UEFA), Europa pamoja na European Conference League baada ya kuitoa Leicester City kwa jumla ya mabao 2-1 na kufanikiwa kutinga fainali ambayo itachezwa Mei 25, 2022 dhidi ya Feyenoord ya nchini Uholanzi.

Mashabiki wa AS Roma wakishangilia timu yao kutinga katika Fainali ya Kombe la Europa Conference League

Mourinho amefanikiwa kuchukua Kombe la Uefa mara mbili akiwa na vilabu vya FC Porto pamoja na Inter Milan huku akifanikiwa pia kutwaa Kombe la Europa akiwa na Klabu ya Manchester United baada ya kuichapa Ajax Amsterdam na sasa amefanikiwa kutinga fainali ya Europa Conference League ambapo kama akifanikiwa kutwaa taji hilo basi ataweka rekodi ya kipekee ya kuwa Kocha pekee aliyetwaa mataji matatu ya mashindano yote yaliyoandaliwa na UEFA.

Leave A Reply