Nape Amuomba Radhi Magufuli – Video

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye,  akimuomba radhi Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John  Magufuli.

 

MBUNGE wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, leo Septemba 10, 2019,  amekutana na kumuomba radhi Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kufuatia kuhusika kwake katika mazungumzo dhidi yake.

“Nilikuja kumuona kama Baba yangu, Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu, kwasababu wote mnajua yametokea mambo mengi hapa katikati na mimi kama Mtoto wa CCM, kama Mwanae nilisema nadhani ni vizuri nije niongee na Baba yangu, na ameniambia kwamba amenisamehe na amenipa ushauri kwa kweli namshukuru sana,” amesema Nape.

 

“Ameeleza hata baadhi ya watu ambao walikuwa wanamuhubiri, wengine wapo kwenye Chama lakini nimesema yote nasamehe, huyu bado ni kijana mdogo ana future nzuri katika maisha yake, nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu ni dhambi kubwa kwa Mungu,tumefundishwa tusamehe.

“Nape amekuwa akiniandikia meseji nyingi tu za kuomba msamaha, amefika kwa viongozi wengi tu, mpaka kwa mzee Mangula, kwa mama Maria Nyerere akieleza nia yake ya kuniomba msamaha, hata wasaidizi wangu wamepata taarifa zake. Leo akasema anataka kuniona, nikaona nimruhusu aje.

“Tunafundishwa katika maandiko kusamehe saba mara sabini, mimi nimemsamehe kabisa kwa dhati ya moyo wangu, akafanye shughuli zake vizuri, akalee mke wake na watoto wake, akawatumikie wananchi wa jimbo lake na chama chake kwa moyo mweupe,” amesema Magufuli.


Loading...

Toa comment