The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MBUNGE ZUBERI WA CUF AHAMIA CCM – VIDEO

Mbunge wa Liwale, Lindi kwa tiketi ya CUF, Zuberi Kuchauka ametangaza kukihama chama hicho leo Agosti 13, 2018 na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijijini Dar.

“CCM hii nimeikubali kwa sababu imerejea katika misingi ya TANU na mimi kama Mtanzania mpenda maendeleo sikusita kurejea, Mimi sisemi kwamba nahamia CCM, ni nimerejea CCM. Narejea CCM nikiwa na uhakika kwamba CCM niliyoiacha mwaka 2005 si hii ya leo” amesema Zuberi Kuchauka.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.