The House of Favourite Newspapers

Breaking: Membe Awasili Dodoma Kuhojiwa na CCM – Video

0

WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe,  leo asubuhi Alhamisi Februari 6, 2020, amewasili katika ofisi za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili.

Membe amewasili katika ofisi hizo maarufu kama ‘White House’ akiwa katika gari aina ya Range Rover jeusi.

Baada ya kuwasili, akiwa amevaa suruali nyeusi na shati lenye michirizi mieusi na kijani, alisalimiana na watu mbalimbali aliowakuta nje, kisha kuingia ndani ya jengo hilo lililopo katikati ya Jiji la Dodoma.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyoketi Desemba 13, 2019 iliagiza makada watatu wa chama hicho waitwe na kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kwenda kinyume na taratibu za chama.

Wengine ambao wanapaswa kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM ni makatibu wakuu wa zamani wa chama hicho tawala nchini, Abdulrahman Kinana na Yussuf Makamba.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply