Breaking: Mgombea Mwenza wa Urais Anusurika Kifo kwa Ajali Mbaya

Gari alilokuwa akiitumia Mgombea Mwenza wa Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Salum Mwalimu limepata ajali mbaya eneo la Msoka Kata ya Ngogwa, Jimbo la Masalala leo Jumatatu, Septemba 21, 2020.

Taarifa iliyotolewa na Chadema imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea wakati wakitoka kwenye mkutano wa Kampeni jimbo la Msalala tukienda kwenye mkutano wa Kahama mkoani Shinyanga.

Taarifa imeendelea kueleza kuwa, ndani ya gari hilo lenye namba T 555 DEP, alikuwemo Mgombea mwenza, Mhe. Salum Mwalim, Katibu wa Makamu wa Rais, Gerva Lyenda, Mlinzi, Omary na Dereva, Haule.


Aidha, gari hiyo imeelezwa kuwa imepinduka na kazunguka mara tano, lakini paka sasa wote tupo salama. Endelea kufuatilia taarifa zetu.

Toa comment