The House of Favourite Newspapers

Breaking: Morrison Ashinda Kesi yake Dhidi ya Yanga -Video

0

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema Bernard Morrison ameshinda kesi yake dhidi ya Yanga Sc na ataendelea kuwa mchezaji halali wa Simba Sc baada ya mapungufu kukutwa kwenye mkataba baina ya Yanga Sc na Morrison.

 

Morrison anapelekwa kwenye Kamati ya Maadili ili kuhojiwa kwa kosa la kusaini mkataba wakati kesi yake ya msingi dhidi ya Yanga ilikuwa haijaanza kusikilizwea wala kutolewa maamuzi.

 

“Kwa kifupi tumegundua kuwa mkataba ulikuwa na uwalakini kidogo na kwamba tunampa faida Morrison kwa maana kwamba tumegundua mkataba wa Yanga una utata. Mapungufu makubwa ambayo tumeyaona ni tarehe ya mkataba, tarehe ya mkataba inaonesha ilisainiwa Machi 20, 2020 wakati tarehe sahihi inaonesha Julai 17, 2020 pia ukurasa wa kutia sahihi umekatwa.

 

“Kesi imemalizika lakini kamati imependekeza apelekwe Kamati ya Maadili kwa sababu amefanya kosa la kusaini mkataba na timu nyingine wakati sisi bado hatujatoa maamuzi,” Elias Mwanjala, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Wachezaji.

 

Imeonekana amesaini Machi 20 na mwingine Julai 15, hivyo mkataba huo ulikuwa na mapungufu, lakini kama Yanga ikihitaji kukata rufaa kama haijaridhika inaweza kwenda CAS,” amesema.

Leave A Reply