The House of Favourite Newspapers

Breaking: NEC Yateua Madiwani Wapya

0

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewateua madiwani watatu wanawake wa viti maalum, kuziba nafasi zilizokuwa wazi kutokana na vifo vya madiwani wa halmashauri hizo.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera walioteuliwa ni Magreth Kaduma ambaye anakuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, akiziba nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa halmashauri hiyo, Mwamini Wikesi.

 

Wengine ni Victoria Ndaki anayekuwa diwani wa viti maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, akiziba nafasi ya Rehema Manangwa aliyefariki dunia na Rhoida Chengula anayekuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, akiziba nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Theresia Kiswaga.

 

Leave A Reply