The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Baada ya IGP Sirro Kuzuru Pwani, Askari Mgambo Mwingine Apigwa Risasi Mkuranga

0

 

MKURANGA: Askari mgambo aliyetambulika kwa jina la Nurdin Kisinga amepigwa risasi leo June 7, 2017 majira ya saa 9 mchana katika Kijiji cha Songa, Mkuranga

Tukio hilo la kinyama limetokea ikiwa saa chache baada ya IGP Simon Sirro kuzuru ukanda huo unaoongoza kwa mauaji ya raia yenye utata.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha mtu huyo kupigwa risasi na amesema majeruhi amelazwa Hospitali ya Songa, Mkuranga     

Kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa mtu huyo amekufa, Kamanda Lyanga amesema anayeweza kuthibitisha kama amekufa au laa, ni daktari lakini taarifa alizonazo yeye ni kwamba amejeruhiwa kwa risasi.

Mtu mwingine, Eric Mwarabu ambaye alikuwa ni askari mgambo, jana usiku alipigwa risasi na kuuawa akiwa amejificha kwenye uvungu wa kitanda nyumbani kwake.

Leave A Reply