The House of Favourite Newspapers

Ajali Mbaya: Basi Lenye Abiria Lateketea

 

ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Tahmeed wamenusurika kupoteza maisha baada ya basi hilo aina ya Yutong kuteketea moto leo mchana Kijijini Matumbi wilaya ya Handeni mkoani Tanga. 

 

 

Kamanda wa Polisi wilaya ya Handeni, William Nyero, amesema basi hilo lilikuwa likitokea Dar es salaam kwenda Mombasa na hakuna madhara kwa binadamu.

 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara. 

 

 

“Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiria ambao walikuwepo kwenye basi hilo wote, waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima”, alisema Kamanda Wakulyamba.

 

BREAKING DKT SLAA USO KWA USO NA MAGUFULI

Comments are closed.