The House of Favourite Newspapers

Chadema: Lissu Amezinduka na Anaendelea Vizuri

0
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali tukio la Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana Alhamisi, mchana.

 

Lissu akipelekwa Nairobi.

Akizungumza na wanahabari leo, Naibu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Safari amesema kuwa chama chao kinalaani tukio hilo kuwa ni la kinyama ambapo amesema serikali haitakiwi kulifumbia macho hata kidogo.

Amesema siku za hivi karibuni Lissu alitoa taarifa kwa wanahabari kuhsu gari linalomfatilia na kwamba watu hao ameshawabaini lakini jeshi la polisi halikuchukua hatua.

Gari la Lissu lilivyofyatuliwa risasi.

Aidha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti  wa Chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Tundu Lissu amezinduka leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya Aga-Khan jijini Nairobi nchini Kenya,  kwa sasa ameshazinduka anajitambua na anaendelea vizuri.

Tundu Lissu.

Pia ameeleza kuwa ifike wakati hawa watu wanasemekana hawajulikani huku wakiendelea kufanya matukio ya kinyama kwa wananchi, watafutwe na wakamatwe.

“Ifike wakati hawa wasiojulikana sasa wajulikane, walimtesa Dkt. Ulimboka, walimmwagia tindikali Kubenea, walimuua mawazo, wakamteka Ben Saanane, Nay wa Miteno na ROMA. Walimtolea bastola Mhe. Nape Nnauye, sasa Watanzania tuseme hatukubali haya yaendelee,” alisema Dk. Mashinji.

Pia ametaja AKAUNTI YA KUCHANGIA MATIBABU YA MHE. TUNDU A. LISSU NI CRDB BENKI/ TAWI LA MBEZI JINA LA AKAUNTI NI : CHADEMA M4C 01J1080100600

Leave A Reply