The House of Favourite Newspapers

Familia ya Yamjibu Sirro Kuhusu Dereva wa Lissu, Yataka Amfuate Nairobi – Video

0
Kaka wa Tundu Lissu.

FAMILIA ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, imehoji kitendo cha polisi kutokumfuata dereva wa Lissu jijini Nairobi badala yake wanamsubiri Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kaka wa Lissu, Alute Mughwai Lissu amehoji inawezekana vipi polisi wasimamishe shughuli kwa sababu ya mtu mmoja?

“Tunashauri polisi wapeleke mpelelezi kule wakachukue maelezo yake badala ya kusubiri arudi,”

Alute amesema hayo kufuatia kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kusema wanaendelea na upelelezi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

IGP Sirro akizungumza akiwa ziarani mkoani Mtwara alimtaka dereva wa Lissu kulisaidia jeshi hilo katika kukamilisha upelelezi. Lissu ambaye anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Alisema miongoni mwa wanaohitajika kwa kuhojiwa ni dereva wa Lissu ambaye inaelezwa yuko Nairobi anakopatiwa matibabu ya kisaikolojia.

“Yule kijana kwenye picha ukimwona yuko vizuri tu, sasa wanaposema anapata huduma ya kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana, hii inatupa changamoto. Ndugu zangu, mheshimiwa Lissu amepigwa risasi na watu tunaowatafuta, huyo kijana aje. Kuja kwake kutatusaidia kupata majibu ya mambo mengi,” alisema IGP Sirro.

VIDEO YA KAKA WA LISSU AKIFUNGUKA

Leave A Reply