The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: Lori Lagonga Gari Tatu Mkoani Mbeya

Usiku wa leo kumetokea ajali mkoani Mbeya katika eneo la Uyole ambapo Lori limegongana na gari ya Coca na kuilalia gari ingine aina ya Noah.

Ajali hiyo imehusisha magari matatu imetokea kwenye mteremko wa mlima Igawilo na kwa mujibu wa mashuhuda gari lenye kontena limeliangukia gari aina ya Noah iliyokuwa na abiria na inasadikiwa watu wanne wamepoteza maisha.

Ajali hii imetokea ikiwa ni saa chache baada ya Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutembelea Mbeya na kutangaza kuvunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na Kamati zake zote za Mikoa na Wilaya.

 

: Zoezi la kuopoa miili ya watu waliokufa kwa ajali iliyohusisha magari matatu usiku wa kuamkia leo jijini Mbeya limekamilika. Imethibitishwa kuwa watu waliokufa ni watano na majeruhi ni mmoja.

Comments are closed.