The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mafuriko ya Mvua Jangwani – Dar, Hali Inatisha

0
Abiria wakichugulia madirishani hali ilivyo wakati mabasi ya mwendokasi yakiwa yamepaki .

MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam tangu juzi Jumanne zimesababisha mafuriko makubwa katika Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ambapo maji yamejaa na kuifunga kabisha barabara hiyo.

 

Mtangazaji wa Global TV Online, Faelister Massae akitimiza majukumu yake eneo la tukio.

Global TV Online imetia kambi eneo hilo na kujionea mabasi ya mradi wa mwendokasi yakiwa yamepaki katikati ya barabara baada ya kushindwa kupita kutokana na mafuriko hayo. Magari yanayotokea upande wa Kimara kuingia katikati ya jiji yameshindwa kuvuka eneo hilo, halikadharika yanayotoka katikati ya jiji kuelekea Kimara na kwingineko yameshindwa kuvuka kuendelea na safari zake kwa saa zaidi ya tatu.

Hali ilivyo eneo la tukio.

Wakizungumza na Global TV Online eneo la tukio, madereva wa mabasi hayo na magari mengine wamesema wanasubiri maji yapungue barabarani ndipo waweze kuvuka kwani wakilazimisha kuvuka ilihali maji yamejaa wanaweza kupata madhara makubwa zaidi.

Mabasi ya mwendokasi yakiwa yamepaki katikati ya barabara baada ya kushindwa kuvuka.

Kwa upande wao madereva bodaboda nao wameleeza kuwa hawawezi kuvuka kwani maji ni mengi kuliko kawaida. Abiria wao wameishushia lawama mamlaka inayohusika na ujenzi wa barabara hiyo wakieleza kuwa, wakati wa ujenzi wa barabara hiyo awamu ya pili walipaswa kuiinua juu kwani ipo chini hivyo mvua zikinyesha maji yanajaa na kusababisha maafa.

Hakuna kifo, majeruhi wala maafa makubwa yaliyoripotiwa kutokana na mafuriko hayo mpaka sasa.

Mwanzoni mwa mwaka huu, mvua kama hizi zilinyesha na kusababisha mafuriko makubwa eneo hilo ambapo mtu mmoja alisombwa na maji na kusababisha kifo papo hapo.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

===

TAZAMA HAPA TUKIO KAMILI

Leave A Reply