The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mahujaji wa Mecca Watapeliwa Dar, Wakwama Airport

0

Mahujaji wa Mecca

 

BAADHI ya mahujaji waliokuwa wamejiandaa kwa ajili kwenda Mecca nchini Saudi Arabia, wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar kufuatia visa, passport na tiketi zao kutokuwa tayari kwa ajili ya safari hiyo.

Wakizungumza LIVE na Global TV Online, mahujaji hao wamesema walitakiwa kuondoka hapa nchini kuelekea Mecca na ndege ya saa 8 mchana lakini cha kushangaza imeshindikana kwa kuwa taasisi walioilipa fedha ili kuwakamilishia taratibu zote za safari hiyo viongozi wake wameingia mitini na kuwaachia mabegi matupu.

Mahujaji hao wanaeleza kusikitishwa kwao na kile walichokiita kuwa ni utapeli huku wakifanya kila jitihada za kuwasiliana na viongozi wa taasisi hiyo lakini simu zao hazipokelewi na wengine zinapokelewa na wafanyakazi wao wa ndai huku wakiwaeleza kuwa wahusika wa simu hizo hawapo jambo ambalo wameshindwa cha kufanya, hivyo wameamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa.

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply