BREAKING NEWS: MAKAMBO ATIMKA YANGA, AJIUNGA HOROYA AC

TAARIFA zilizosambaa kwa kasi mitandaoni zinaeleza kuwa Klabu ya Horoya AC ya nchini Guinea imemsajili mshambuliaji matata wa Klabu ya  Yanga ambaye ni raia wa DR Congo, Heritier Makambo, leo Alhamisi, Mei 16, 2019.

 

Imeelezwa kuwa Makambo amejiunga na miamba hao wanaoongoza Ligi Kuu ya Guinea wakiwa na pointi 49 baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

 

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amethibitisha taarifa hizo na kusema taarifa alizokuwa nazo awali ni kwamba  Makambo alikwenda Guinea kwa ajili ya kufanya vipimo wala si kusaini mkataba moja kwa moja.

 

Loading...

Toa comment