Simba waweka kikao cha Niyonzima, Kapombe

UONGOZI wa Simba umeanza rasmi mazungumzo na nyota wake ambao mikataba yao inaelekea kumalizika mwisho wa msimu huu wakianza na Shomari Kapombe na Haruna Niyonzima.

 

Simba ambayo ipo katika harakati za kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara, kwa msimu wa pili mfululizo, itakutana na benchi la ufundi ili kujua mahitaji ya kocha wao Patrick Aussems.

 

Chanzo makini kimeliambia Championi Jumatano kuwa, kikao hicho kilifanyika ndani ya Hoteli ya Seascape, Mbezi Beach jijini Dar, na kumtaka kocha na wenzake kuweka wazi mipango yao ya ubingwa msimu huu na msimu ujao ambapo alipendekeza baadhi ya nyota wake kama Niyonzima na Kapombe waongezewe mikataba mipya.

 

“Kweli kocha ametaka wachezaji wote waliokuwa majeruhi mwanzo wa ligi na wamerejea na kuonyesha uwezo mzuri kama Niyonzima, Kapombe na wengine walioshiriki vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya waongezewe mikataba kabla hawajaanza usajili wa wengine wapya.

 

“Kwa ujumla uongozi ulikaa kikao kujadili suala hilo na umemuelewa kocha na kuanzia wiki Ijayo utaanza rasmi kufanyia kazi mawazo yake yote ili waweze kujipanga mapema kwa msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi baada ya kupata taarifa hizo lilimtafuta Niyonzima ili azungumzie kama yupo tayari kuongeza mkataba ambapo, alisema:

 

“Nina mipango mingi sana msimu ujao ingawa kila mchezaji mzuri hupenda kufanya kazi sehemu moja bila kuhama, hivyo endapo watanitaka niongeze mkataba, nitawasikiliza na tukiafi kiana bila vikwazo na wakikubaliana na mahitaji yangu nitasaini,” alisema Niyonzima.

Musa Mateja, Dar es Salaa

Loading...

Toa comment