The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Malinzi, Mwesigwa Wanyimwa Dhamana, Warudishwa Rumande

0
Jamal Malinzi na Celestine Mwesigwa wakiwa mahakamani Kisutu leo wakizungumza na mmoja wa wanasheria wao.

 

#GlobalHabari: Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa wamefikishwa tena mahakani Kisutu na kusomewa mashataka ya rushwa yanayowakabili.

Watuhumiwa hao wamenyimwa dhamana na kurejeshwa tena mahabusu hadi Julai 17, mwaka huu.

 

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).
Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

 

Aidha TAKUKURU imewapandisha tena katika Mahakama ya Kisutu, Dar, mmiliki kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh na mfanyabiashara James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi.

 

Leave A Reply