The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Droo Ndogo Ya 5… Yavutia Wadhamini Zaidi

0
Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub (kushoto) akimuelekeza Benjamin Chimenya kuzaja kuponi ya Shinda Nyumba.

 

WAKATI maandalizi ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili droo ndogo ya tano yakiendelea, Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Premier Bet, imejitokeza na kuwa miongoni mwa wadhamini wa tukio hili kubwa kuwahi kutokea nchini.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa, Championi, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda, Yohana Mkanda, alisema wadhamini hao wameongezeka ili kutoa fursa zaidi kwa wasomaji wa magazeti hayo ambao wanashiriki zoezi hilo.

Aisha Ajibu kushoto, Mr. Shinda Nyumba, Hawa Ajibu na Mama Mrangi wakiwa kwenye pozi.

 

“Hili ni shindano kubwa ambalo linawahusisha watu wengi, kadiri muda unavyokwenda idadi ya watu wanaoshiriki inaongezeka, ndiyo maana Premier Bet wakaona nao watie mguu. Huu ni wakati muafaka kwa wasomaji kuendelea kupata kuponi ili waweze kufaidika na udhamini wao,” alisema Mkanda.

Mkanda alitoa maelezo hayo wakati droo ndogo ya tano ikiwa katika maandalizi kwani Julai 20 mwaka huu itachezeshwa tena.

 

 

Katika droo ndogo nne ambazo zimeshachezeshwa, washindi waliopatikana walipata zawadi za pikipiki, televisheni kubwa ‘Flat Screen’, simu za kisasa za mikononi, vyombo vya nyumbani, Ving’amuzi vya Ting na zawadi nyingine ndogondogo.

Ofisa Masoko huyo wa Global Publishers ambao ndiyo waendeshaji wa Bahati Nasibu hiyo, alikiri kutumika kwa mamilioni ya shilingi hadi sasa wanapojiandaa kwa droo ndogo ya tano.

“Tumetumia fedha nyingi sana hadi hivi sasa, kwa sababu kama wasomaji wenyewe wanavyojua zawadi tunazotoa ni zenye thamani ya mamilioni ya shilingi, hii yote ni kuwaonyesha wasomaji ni kwa jinsi gani Global Publishers inawajali wasomaji wake,” alisema.

 

“Tumedhamiria kuboresha zawadi zetu kwa washindi wa droo ndogo ili kuhakikisha zinakwenda na wakati, ni wakati wa wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa, Championi, Amani, Uwazi, Risasi na Ijumaa Wikienda kuendelea kununua nakala zao na kujaza kuponi ili waweze kujaribu bahati zao,” alisema.

Washindi zaidi ya 20 wameshapatikana hadi sasa kwenye bahati nasibu hiyo ambao walibadilisha maisha yao kwa zawadi walizojipatia.

 

 

 

Droo ndogo ya tano inatarajiwa kufanyika Julai 20, mwaka huu katika eneo ambalo bado linafanyiwa kazi.

Mkanda alisema jana kuwa bado wanaendelea na mikakati ya kuboresha zawadi wakati huu muda wa kumpata mshindi wa zawadi kubwa ya nyumba ukiendelea kukaribia.

Ukiacha Premier Bet, wadhamini wengine wa bahati nasibu hii ni Kampuni ya Tecno Mobile na Kampuni ya Ving’amuzi vya Ting.

 

NA MWANDISHI WETU | WIKIENDA

Leave A Reply