The House of Favourite Newspapers

Mawaziri sita waapishwa Ikulu, Dar!

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Gerson Lwenge kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akimuapisha Profesa Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasilina Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akimuapisha Prof. Makame Mbarawa baada ya kumhamisha kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda kuwa Waziri katika Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akimuapisha Mh. Hamad Masauni kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha mawaziri na naibu waziri, Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli aliwateua mawaziri na naibu waziri hao Desemba 23 ili kukamilisha idadi kwenye Baraza la Mawaziri.

Walioapishwa leo ni

Prof. Jumanne Maghembe -Waziri wa Maliasili na Utalii.
Dkt. Philip Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
Eng. Gerson Lwenge – Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Dkt. Joyce Ndalichako – Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
Mh. Hamad Masauni –Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Prof. Makame Mbarawa –Aliyehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Leave A Reply