The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mkutano wa Nape Wajaa Figisu, Aongelea Barabarani, Apongeza Uamuzi wa Rais Magufuli

KUFUATIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo kutengua uteuzi wa Waziri  wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo, Nape Nnauye na nafasi kuchukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe, Nape amefanya mkutano na waandishi wa habari licha ya mkutano huo kujaa figisu kibao.

Asubuhi Nape aliandika kupitia Twitter kwamba angefanya mkutano na wanahabari katika Hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay Jijini Dar, baada ya wanahabari kuwasili hotelini hapo uongozi wa hoteli hiyo uliwatarifu kuwa mkutano wa Nape hautakuwepo kwani umezuiliwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni.

 

Wanahabari walimsubili Nape mpaka alipowasili na kufanya nao mazungumzo akiwa kwenye gari lake barabarani.

“Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia.”

“We have nothing to fear, but fear itself.”

“Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola.”

“Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu.Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo.”

“Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.

 

“Kina Mwalimu Nyerere, Kawawa na wengine walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?”

“Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka.

“Namshukuru Rais kwa mwaka 1 alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.”

“Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali.”

“Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.” alisema Nape Nnauye.

Gari la Nape limezuiwa kutoka ambapo inaonekana gari ya Kamanda wa Polisi Kinondoni limefunga barabara.

 

NA HIKI NDICHO ALICHOKIZUNGUMZA

Picha na Mussa Mateja/GPL

Comments are closed.