The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Msanii Jebby afariki dunia kwao Dodoma

Msanii Jebby amefariki dunia leo nyumbani kwao huko Dodoma ambapo taarifa zinasema alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye bandama.

Msanii Jebby atakumbukwa kwa wimbo wake wa ‘Swahiba’ aliomshirikisha Afande Sele.

Mdogo wake Jebby amethibitisha kifo cha kaka yake na kusema alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye bandama na upungufu wa damu.

Wiki iliyopita Jebby aliomba kurudishwa kwao Dodoma baada ya hali yake kubadilika.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Comments are closed.