The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mtendaji wa Kijiji Auawa Kibiti, Nyumba ya Mwenyekiti Yachomwa Moto

0

 

KIBITI: Viongozi wawili wamepigwa risasi katika Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).

Waliopigwa risasi wametajwa kuwa ni Ofisa Mtendaji wa Kiijiji, Shamte Rashidi Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus huku nyumba yake ikachomwa moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa tukio hilo.

Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi hivyo watatoa taarifa rasmi za tukio hilo baadaye.

Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi. 

Leave A Reply