The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Polisi, Vijana Wapambana Bomoa-Bomoa Jangwani, Dar

0

Mwonekano wa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo ubomoaji wa nyumba zilizokuwa eneo hilo ambalo ni bonde, ulikuwa ukiendelea.  Tukio hilo lilisababisha makabiliano ya uhasama kati ya polisi na vijana waliokuwa wanawarushia mawe polisi wakipinga nyumba hizo zisibomolewe.
Polisi wakiwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani wakati wa ubomoaji wa nyumba ambazo ziko katika bonde hilo .
Wakazi wa Dar es Salaam wakiwa katikati ya Barabara ya Morogoro wakishangaa basi la mwendo kasi lililovunjwa kwa mawe na wanaodaiwa kuwa vijana waliokuwa wanapinga bomoabomoa iliyokuwa ikifanyika eneo la bonde la Jangwani.
Kituo cha mabasi ya mwendo kasi eneo la Jangwani, Barabara ya Morogoro, kikiwa kimevunjwa katika vurugu za leo.

 

NYUMBA  zilizopo eneo la bondeni Jangwani jijini Dar es Salaam, zimeendelea kubomolewa leo na kikosi maalum huku vijana wasiofahamika wakidaiwa kuwarushia mawe polisi wakipinga ubomoaji wa nyumba hizo.  Katika tukio hilo polisi walichukua hatua za kuwadhibiti vijana hao.

Miili ya Watanzania 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Yaagwa Lugalo

Leave A Reply