The House of Favourite Newspapers

Shilole Ahukumiwa kwa Utapeli, Mahakama Kukamata Mali Zake! – Video

Shilole akiwasili mahamani hapo.

MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

…Akiwa na mumewe Uchebe.

Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu kwa Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

…Akiingia ndani ya chumba cha mahakama.

Kutokana na kitendo hicho,  mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo hivyo kumsababishia mwandaaji ambaye ni Mary, hasara ya Tsh. Milioni 14 ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.

Mlalamikaji Mary Mussa.

 

Baada ya tukio hilo, Mary alifungua kesi mahakamani hapo akiomba kulipwa kiasi hicho cha fedha kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na Shilole kushindwa kufika lakini msanii huyo anadaiwa kupuuza wito wa mahakama.

 

Shilole, Uchebe na wakili wao.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya hivyo hadi mahakama ilipomuandikia wito mwingine kwenye Gazeti la Uhuru lakini hakufika pia.

 

 

Shilole akiangua kilio.

 

Shilole aliambatana mahakamani hapo na mumewe, Uchebe,  na wakili wake ambaye baada ya kufuatwa kwa mahojiano na Global TV, alikataa kutaja jina lake wala kuzungumza chochote kuhusu kesi hiyo.

Wakiwa na wakili.

 

Mahakama imemuamuru azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.

KUTOKA GAZETI LA UHURU

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

BREAKING: Shilole Kahukumiwa! Mahakama Kuuza Mali Zake!

 

SHILAWADU Walivyotibua Harusi ya Shilole

Comments are closed.