Kartra

Breaking News: Treni ya Abiria Yapata Ajali Kilosa

Treni ya abiria imepata ajali eneo la Kidete mpakani mwa Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro na Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma leo Alhamisi, Julai 22, 2021.

Habari kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo akiwa ameongozana na maofisa wengine, wanaelekea eneo ilipotokea ajali hiyo.

Taarifa za awali zinadai chanzo cha ajali hiyo ni gari kuigonga treni hiyo ya abiria na mpaka sasa bado haijfahamika madhara yaliyotokana na ajali hiyo.

Taarifa zaidi endelea kutufuatilia.

 

 

 


Toa comment