The House of Favourite Newspapers

Breaking: Ninja Asaini Miaka Miwili Yanga

0

BEKI wa kati Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ leo Agosti 6 amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga.

Ninja msimu wa 2017/18 alikuwa anakipiga ndani ya klabu hiyo alipata timu Serbia iliyokuwa inaitwa MFK Vyskov iliyomtoa kwa mkopo akacheze ndani ya Klabu ya LA Galaxy nchini Marekani.

 

Baadaye alirudi tena kwenye Klabu yake ya MFK Vyskov ambako alikosa nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza jambo lililomfanya arejee nyumbani Tanzania.

Alianza majaribio ndani ya Yanga chini ya Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye amefutwa kazi Julai 27 na hatimaye leo ametambulishwa rasmi kurejea kwenye timu yake ya zamani.

 

Huu unakuwa ni usajili wa tano kwa Yanga ambayo ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi ikiwa imemalizana na Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki kutoka Coastal Union, Zawadi Mauya kiungo kutoka Kagera Sugar, Yasin Mustapha beki kutoka Polisi Tanzania na Wazir Jr mshambuliaji kutoka Mbao FC.

Leave A Reply