The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Yakutana na Wasomaji Wake

0
Msomaji huyu alinaswa maeneo ya Mwenge akipata burudani ya Spoti Xtra.

Kikosi cha Masoko na Usambazaji cha Magazeti ya Global Publishers watoaji wa gazeti la Spoti Xtra leo kimeingia mtaani na kuzungumza na wasomaji wa gazeti hilo na kupata maoni yao.

Vijana wa Kijiwe cha bodaboda cha Mtaa wa Mabatini, Kijitonyama Dar wakiwa makini na magazeti ya Spoti Xtra baada ya kutembelewa na kikosi cha mauzo na masoko.

 

Washkaji wa Tandale Uzuri wakipitia Spoti Xtra.

Kikosi hicho kikiongozwa na mkuu wa kitengo hicho, Anthony Adamu kiliizunguuka pande mbalimbali za jiji la Dar ikiwemo maeneo ya Ubungo, Mwenge, Tandale, Mwananyamala, Kijitonyama na kwingineko.

 

Dereva wa bodaboda wa Ubungo Mawasilino akielezea kinachomfanya asikubali kupitwa na Spoti Xtra.

Katika mizunguuko hiyo kilikutana na wasomaji hao na kuwauzia gazeti la Spoti Xtra ambalo waliendelea kulimwagia sifa lililosheni habari habari za michezo, hadithi za kusisimua, makala za michezo na mambo mengine ya kuvutia.

Afisa Masoko, Songoro Bilal akizungumza na wasomaji aliokutana nao Sinza White Inn, Dar.

Wasomaji hao pamoja na kutoa pongezi za ubora wa gazeti hilo nao walitoa mapendekezo yao kwa mambo waliyotaka yaongezwe na mengine kupunguzwa.

Maoni hayo yaliyotolewa na wasomaji hao yalichukuliwa kitengo hicho na kuwaahidi wasomaji hao kuyafanyia kazi kama walivyoyawasilisha.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply