The House of Favourite Newspapers

Breaking: Rufaa Ya Mbowe, Matiko Kuendelea Kesho (Picha +Video)

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa ndani ya gari la Magereza.

 

RUFAA ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko kupinga kufutiwa dhamana leo imekwama kusikilizwa.

 

Rufaa hiyo imekwama kusikilizwa kutokana na kukosekana kwa mwenendo na uamuzi wa kuwafutia dhamana, hivyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupanga kusikilizwa kesho ili Jaji Rumanyika anayesikiliza  kesi hiyo asome mwenendo wa uamuzi wa kufutiwa dhamana.

Freeman Mbowe na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko wakisalimia walipofikishwa mahakamani hapo leo.

Miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliofika mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika, wabunge na madiwani.



 

 

 

Comments are closed.