The House of Favourite Newspapers

Zitto Kabwe Aungana na Chadema Rufaa Ya Mbowe (Picha+Video)

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakisalimia baada ya kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

 

MBUNGE wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wameshawasili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Jumatano kusikiliza rufaa ya dhamana yao iliyofutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23.

Kiongozi wa chama cha ACTWazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefika katika mahakama hiyo akiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji.

Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji (katikati) akiongea jambo na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Viongozi mbalimbali wa upinzani wakiendelea kujadili mambo mbalimbali.
Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye (kulia) akiongea jambo.

PICHA: DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.