The House of Favourite Newspapers

BREAKING: SOUDY Brown Aachiwa kwa Dhamana, Ashikiliwa – Video

WATU watano wakiwemo Soudy Brown, Shafii Dauda, Sudi Kadio, Benedict Kadege na Michael Mlingwa wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 24, 2018, wakikabiliwa na makosa ya kurusha maudhui kupitia Online TV bila ya kibali.

 

Washitakiwa hao walishuka kwenye karandinga la polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam walikokuwa wameshikiliwa huku wakiwa wamevalia kininja ili kuficha nyuso zao.

Kesi hiyo, ambayo kwa upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili Peter Kibatala akisaidiana na wakili Maghimbi, Soudy Brown anashtakiwa kwa kosa la kurusha maudhui kupitia YouTube akaunti yenye jina la Shilawadu TV ambayo haijasajiliwa lakini alikana mashtaka hayo.

Baada ya Hakimu kusikiliza kesi hiyo, Kibatala aliomba mteja wake apewe dhamana kwa sababu kosa lake linadhaminika, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile alikubali na kutoa masharti ya washtakiwa kuwa na mdhamini mmoja (kila mmoja) kusaini na bondi ya shilingi milioni 2 kila mmoja.

 

Soudy alifanikiwa kukamilisha masharti ya dhamana hiyo, hata hivyo, Soudy Brown bado anashikiliwa na polisi kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 18, 2018.

VIDEO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.