The House of Favourite Newspapers

Breaking: WAFANYAKAZI WA CLOUDS WAPATA AJALI WAKITOKA KUMZIKA RUGE

 

TIMU ya Uzalishaji wa Vipindi wa kituo cha Clouds Media cha Dar es Salaam leo imepata ajali ya gari maeneo ya nje kidogo ya Dodoma ikitoka Bukoba  kumpumzisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba,  ampabo mazishi yalifanyika Machi 3, 2019, nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba.

Habari zilizopo zinasema watu hao wamepata ajali wakiwa  katika gari yao yenye namba za usajili T884 DNS ndani iliyokuwa na watu sita na wote wametoka salama.

Kupitia page yao ya instagram, Clouds TV imesema:  Tunasikitika kuwataarifu kuwa sehemu ya timu yetu ya production (Watu 6) iliyokuwa ikitokea msibani Bukoba kurejea jijini Dar es Salaam imepata ajali ya gari maeneo ya nje kidogo ya Dodoma.

Tunamshukuru Mungu hakuna aliyepata madhara makubwa kutokana na ajali hiyo.
Tunatoa shukrani za dhati kwa mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ndugu yetu Anthony Mavunde kwa msaada wa haraka aliowapatia vijana wetu ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu na vipimo zaidi Jijini Dodoma.
Poleni sana ndugu zetu wa Clouds Media, Mwenyezi Mungu awape wepesi katika hili.

Comments are closed.