The House of Favourite Newspapers

Breaking: Waziri Apigwa Risasi

0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Uganda, Jenerali Katumba Wamala amenusurika kifo baada ya gari lake kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana ambapo dereva wake na binti yake waliokuwa pamoja ndani ya gari hilo, wamefariki dunia.

Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo, majira ya saa tatu ambapo waziri huyo, alionekana akiteremka kwenye gari lake muda mfupi baadaye, huku mavazi yake yakiwa yametapakaa damu.

Waziri huyo baada ya kunusurika, amekimbizwa katika Hospitali ya Malcom na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Medipal anakoendelea kutibiwa.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply