The House of Favourite Newspapers

Bupandwa mguu sawa kuwavaa Nyanzenda Shigongo Cup Buchosa

0

Yale mashindano ya Shigongo Cup yaliyokuwa yakifanyika kwa kushirikisha jumla ya timu 22 yanatarajiwa kufika tamati wikendi hii ambapo timu za Bupandwa FC na Nyanzenda FC zinatarajia kumenyana  katika fainali ya mashindano hayo iliyopangwa kuchezwa septemba 9 kwenye uwanja wa Kalebezo Buchosa mkoani Mwanza.

Bupandwa fc walitinga hatua ya fainali baada ya kupata ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Bangwe huku Nyanzenda wao wakifika hatua ya fainali baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 mbele ya Kalebezo FC.

Mratibu wa mashindano hayo Marco Zagaro amesema “ Mashindano yetu ya Shigongo Cup yalianza kwa kushirkisha jumla ya timu 22 ambazo zilitokana na kata zilizopo kwenye jimbo letu la Buchosa na ushindani ulikuwa mkubwa na vipaji vilionekana ambo ambalo limepelekea timu bora za Bupandwa na Nyanzenda kukutana ili kucheza fainali” alisema

Bingwa wa Shigongo jimbo Cup atapewa zadi ya fedha taslimu shilingi 1500,000, mshindi wa pili atalipwa 700,000 na mshindi wa tatu atapewa 350,000 na wale wachezaji wote ambao wameonekana kufanya vyema katika mashindano watatafutiwa nafasi ya kucheza soka la kulipwa kwenye vilabu mbalimbali hapa nchini.

 

 

 

Leave A Reply