Job Avunja Rekodi Yake Yanga, Afunga Bao Katika Mchezo Wake wa Kwanza
DICKSON Job, beki mzawa ndani ya kikosi cha Yanga, amevunja rekodi yake aliyoaindika msimu wa 2022/23 kwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza.
ob msimu wa 2022/23 alikamilisha akiwa ametupia bao moja baada ya kucheza mechi 24 na kukomba dakika 2,025, chini ya Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambapo Yanga ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kazi imeanza kwa mara nyingine msimu mpya Yanga ikiwa chini ya Miguel Gamondi raia wa Argentina ambapo Job ameanza balaa lake mapema.
Mchezo wa kwanza Job alifungua akaunti ya kucheka na nyavu dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.
Job kafungua akaunti dakika ya 16, huku akicheza mechi mbili za ligi akikomba dakika 180.
STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA